20 Mei 2017 - 20:11
Sayed Hasan Nasrullah ampongeza Rais Rouhani kwa ushindi aliopata

Katibu mkuu wa chama cha Hizbullah nchini Lebanon ametuma ujumbe wa kumpongeza Hasan Rouhani kwa ushindi aliopata katuka kinyanganyiro cha kumtafuta Rais wa awamu ya 12 wa jamhuri ya kiislamu ya Iran

Shirka la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: “Sayed Hasan Nasrullah” katibu mkuu wa kikundi cha Hizbullah cha Lebenon katika ujumbe wake kwa Hasana Rouhani, ambapo amepongeza kwa kuchaguliwa kwake kwa mara ya pili kwaajili ya kuongoza jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa miaka minne mingine ijayo.
Kwa mujibu wa ripoti iliosambazwa katika tovuti ya Almanar, Sayed Hasan Nasrullah amesisistiza kuwa kushiriki kwa wananchi wa Iran katika vituo vya kupiga kura, ni jambo linalothibitisha adhama ya jamhuri ya kiislamu ya Iran.
Aidha rais wa Syria na Waurusi pia katika nyakati mbalimbali wametuma ujumbe wa kumpongeza Hasan Rouhani kwa ushindi aliopata katika uchaguzi wa Urai uliofanyika siku ya Ijumaa, ambapo wananchi wa Iran kwa mara nyigine tena kumpa kibali cha kuiongoza Iran kwa miaka minne ijayo.
mwisho/290